Mwenyekiti
Msaidizi wa Tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015 litakaloipigia kampeni
CCM, Wema Sepetu akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam juu
ya tamasha na kampeni zao. Kutoka kulia ni Wellu Sengo (Matilda).
Mwenyekiti
Msaidizi wa Tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015 litakaloipigia kampeni
CCM, Wema Sepetu akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam juu
ya tamasha na kampeni zao. Kulia ni Yobnesh Yusuph (Batuli) na kushoto
ni Steve Mengele a.k.a Steve Nyerere wakiwa katika mkutano huo.
Kada
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mratibu wa Tamasha la MAMA ONGEA NA
MWANAO 2015 litakaloipigia kampeni CCM, Steve Mengele a.k.a Steve
Nyerere akizungumza na waandishi wa habari leo juu ya tamasha hilo.
Mwenyekiti
Msaidizi wa Tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015 litakaloipigia kampeni
CCM, Wema Sepetu (kulia) akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es
Salaam juu ya tamasha na kampeni zao. Kutoka kulia ni Wellu Sengo
(Matilda) na Yobnesh Yusuph (Batuli).
Mwenyekiti
Msaidizi wa Tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015 litakaloipigia kampeni
CCM, Wema Sepetu akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam juu
ya tamasha na kampeni zao. Kulia ni Yobnesh Yusuph (Batuli) na kushoto
ni Steve Mengele a.k.a Steve Nyerere wakiwa katika mkutano huo.
Baadhi
ya wasanii na makada wa CCM ambao watajumuika katika tamasha la MAMA
ONGEA NA MWANAO 2015 litakaloipigia kampeni CCM wakiwa katika picha ya
pamoja mara baada ya mkutano na waandishi wa habari.
Baadhi wa aandishi wa habari wakiwasikiliza wasanii hao na waratibu wa tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015.
………………………………………………………………………………
WASANII ambao ni makada wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM) wameandaa Tamasha kubwa kuzunguka nchi nzima kwa
pamoja na kukinadi chama hicho tawala pamoja na Sera zake ili kiweze
kushinda Uchaguzi Mkuu onaotarajia kufanyika Oktoba Mwaka huu (2015).
Tamasha hilo litakalojulikana
kama “MAMA ONGEA NA MWANAO 2015″ limeandaliwa na baadhi ya wasanii
makada wa CCM wapatao 250 ambao watazunguka mikoa zaidi ya 10 kukipigia
kampeni chama hicho tawala ili kiweze kupewa ridhaa tena na Wananchi ya
kuendelea kuongoza nchi.
Akizungumza leo jijini Dar es
Salaam na waandishi wa habari Mwenyekiti Msaidizi wa tamasha hilo, Wema
Sepetu alisema madhumuni ya tamasha la Mama Ongea na Mwanao 2015 ni
kulinda mazuri yote yalioasisiwa na CCM kupitia viongozi wake akiwemo
Baba wa Taifa Mwalimu Julias Nyerere na Sheikh Abeid Aman Karume.
Msanii Sepetu akiyataja masuala
hayo yalioasisiwa na CCM kupitia viongozi hao kuwa ni pamoja na amani na
utulivu uliopo hadi sasa, maendeleo ya kijamii na kiuchumi yalioletwa
hadi sasa, masuala ambayo yanastahili kuendelezwa na wala si kubezwa.
Tamasha hilo linajumuisha wasanii
kama Odama, Davina, Wastara Juma, Keisha, Wellu Sengo (Matilda), Bi.
Mwenda, Mama Lolaa, Mama Nyamayao, Herieth Chumila, Thea, Maya, Chuchu
Hans, Steve Nyerere pamoja na wasanii wengine wengi.
Aidha alisema kupitia tamasha
hilo wasanii hao pamoja na wenzao watazunguka katika mikoa zaidi ya 10
kwa pamoja kufanya kampeni kumnadi mgombea wa urais kupitia CCM, Dk.
John Pombe Magufuli, mgombea Mwenza, Samia Hassan Suluhu pamoja na
viongozi wengine ngazi mbalimbali wanazogombea kupitia chama cha
Mapinduzi.
Madhumuni ya tamasha la Mama
Ongea na Mwanao 2015 ni kulinda mazuri yote yalioasisiwa na CCM kupitia
viongozi wake akiwemo Baba wa Taifa Mwalimu Julias Nyerere na Sheikh
Abeid Aman Karume ambayo bila amani mama awezi kujifungua salama, Bila
mama hakuna familia, amani inapotoweka mama hawezi kukimbia kilometa
kadhaa na kuiacha familia yake, bila mama hakuna ujasiliamali, mama ni
kimbilio la baba, kaka, dada na watoto…ikumbukwe kuwa mama ndio mpiga
kura ndio maana tunasema mama ongea na mwanao,” alisema Wema Sepetu.
“Na leo hii kuanzia sasa
tunatambulisha kampeni yetu tunayoifanya kuhamasisha vijana, kinamama,
kinababa, mashabiki wetu wale wote wenye sifa za kupiga kura wapige kura
kwa kumchagua kiongozi bora anayetoka Chama Cha Mapinduzi…chagua Dk.
Magufuli, Samia Suluhu, wabunge na madiwani wa Chama Cha Mapinduzi,”
alisema Sepetu.
Aidha wasanii hao wamempongeza
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya
Kikwete kwa kuongoza vizuri vikao vyote vya chama hicho hadi kupatikana
kwa mgombea bora wa urais kupitia chama hicho (Dk. Magufuli), hivyo
kuwataka wanaCCM wote ambao waligombea na hawakupata nafasi kuungana na
kukitumikia chama.
“…Mimi Wema Abraham Sepetu nikiwa
na baadhi ya wasanii wenzangu ambao tuligombea tunasema muda bado tunao
na siku tunazo kwa kukitumikia chama tukipewa ridhaa kwa njia yoyote na
kwa nafasi yoyote ndio maana hatuja teteleka tupo imara kuwatumikia
wananchi katika nafasi nyingine ndani ya CCM,” alisema Sepetu.
Imeandaliwa na www.thehabari.com
Imeandaliwa na www.thehabari.com
P yhaa tv come soon
Tuwe Pamoja Huku Ilikupata Stori ZOTE
share
face book ipyana stephen
Share
Share
instagram p yhaa tv
instagram p yhaa tv
usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

0 comments:
Post a Comment