Meneja
wa Arsenal, Mfaransa Arsene Wenger amesema kuwa kiungo wa klabu yake
Jack Wilshere anatarajiwa kurejea tena dimbani wiki mbili zijazo baada
ya kupata maumivu ya kifundo cha mguu.
Wilshere mwenye miaka 23 aliumia katika
mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya Agosti 1 ambapo ilidhaniwa angekaa
nje ya uwanja kwa miezi miwili, lakini Wenger amesema kiungo huyo wa
kimataifa wa Uingereza anatarajiwa kupona ndani ya muda mfupi ujao.
Wakati huo huo mchezaji mwenzake Tomas
Rosicky aliyefanyiwa upasuaji wa goti anatarajiwa kukaa nje ya dimba kwa
miezi miwili. Akiongea kabla ya kukutana na Crystal Palace katika
mchezo wa jumapili, Wenger alisema ''Jack atakua nje kwa wiki nne na
tiyari zimepita wiki mbili anaendelea vizuri''
Kiungo Rosicky mwenye miaka 34 aliumia
mwezi juni alipokua akiitumikia timu yake ya Jamhuri ya Czech
iliyomenyana na Iceland katika michuano ya kufuzu Euro 2016.
Tuwe Pamoja Huku Ilikupata Stori ZOTE
usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos
Tuwe Pamoja Huku Ilikupata Stori ZOTE
share
Share
Share
instagram p yhaa tv
instagram p yhaa tv
usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

0 comments:
Post a Comment