Stori inasikika kutoka Texas Marekani,
inamhusu mwanaume mmoja aliyeamua kukatisha maisha ya watoto 6, mmoja
ya watoto wao ni mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 13 !!
David Conley amekamatwa
kwa kesi ya mauaji alisema kuwa hakudhamiria kuwaua watoto hao ila
mtoto wake alijenga urafiki na kundi la watoto wenye viburi na aliona
mwisho wa mtoto wake hautokuwa mzuri, alijitahidi kumuonya lakini hakuna
kilichobadilika.
>>>“walikuwa
wanaelekea pabaya, walikuwa hawana heshima, walikuwa waonevu kwa wototo
wenzao… hata Biblia inasema waheshimu baba na mama yako ili siku zako
zipate kuwa nyingi kwenye ardhi ya bwana MUNGU wako, lakini hawa
hawakutii hii amri na sisemi niliwaua kwa sababu hii ila walikuwa hawana
nidhamu… Bibilia inasema usipowaheshimu wakubwa siku zako zitakuwa
fupi duniani”. <<< Hii ni sehemu ya alichokijibu David Conley Mahakamani.
Kesi ya David imepangwa
kusikilizwa tena September 15 ila mpaka sasa mawakili wanaomsimamia
hawajui utetezi wake usimamie upande gani, kwamba alikuwa na kichaa cha
muda ama ana matatizo ya akili!
Tuwe Pamoja Huku Ilikupata Stori ZOTE
share
usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

0 comments:
Post a Comment