Jana
jioni ulichezwa mchezo wa Sports Xtra Ndondo Cup hatua ya 16 bora kati
ya Keko Furniture dhidi ya Buguruni FC mchezo uliomalizika kwa Keko
Furniture kuibuka na ushindi wa goli 2-1 hatimaye kusonga mbele kwenye
michuano hiyo wakati Buguruni FC wao wakiwa wametupwa nje ya michuano
hiyo.
Kitu
cha kuvutia kwenye mchuano huo ni namna ambavyo mashabiki wa Keko
Furniture walivyokuwa wakiishangilia timu yao. Walikuwa ni wengi na
kuwafunika kabisa mashabiki wa Buguruni FC.
“Mimi
sio mganga wala mchawi ila hii ni staili yangu ya kuishangilia timu
yangu, kila mtu anakuja uwanjani kushangilia kwa staili yake mimi
nimeammua kujitofautisha na kuwa na staili yangu ya kipekee ambayo
itanifanya nionekane tofauti kati ya mashabiki wengine”, alisema.
“Hii
inaweza ikawachanga wapinzani wetu kisaikolojia kwamba, Keko Furniture
wamekuja na mganga wao uwanjani kwahiyo wakajua hata wafanye nini leo
hawatoki, na kama tukiwafunga leo lazima utasikia wakisema tumewaroga
ndio maana wamefungwa. Lakini mpira hauna hayo unachezwa uwanjani na
kila mtu anaona”.
P yhaa tv coming soon
Tuwe Pamoja Huku Ilikupata Stori ZOTE
share
face book ipyana stephen
Share
Share
instagram p yhaa tv
instagram p yhaa tv
usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos


0 comments:
Post a Comment