Ripoti kutoka nchini Nigeria
zinasema kuwa karibu watu 60 huenda waliuawa wakati wa shambulizi katika
kijiji kimoja kaskazini mashariki mwa nchini lililoendeshwa na watu
wanaoshukiwa kuwa wanachama wa na Boko Haram.
Shambulizi hilo
lilitokea katika jimbo la Yobe lilifanyika Alhamisi iliyopita na habari
hizo zimepatikana kutoka kwa wale walionusurika.Mwandishi wa BBC nchini Nigeria anasema kuwa ukweli kuwa ilichukua siku tano kabla ya shambulizi hilo kujulikana, ni ishara kuhusu jinsi hali ya usalama ilivyo eneo hilo.
Walioshuhudia walisema kuwa wanamgambo wa Boko Haram waliwasili katika kijiji hicho wakitumia pikipiki ambapo walianza kuwafyatulia watu risasi.
Mikakati ya jeshi Nigeria imelidhoofisha kundi la Boko Haram miezi ya hivi majuzi lakini sehemu zingine za kaskazini mashariki mwa Nigeria kama Yobe na jimbo jirani la Borno yako katika hali mbaya kiusalama.
P yhaa tv come soon
Tuwe Pamoja Huku Ilikupata Stori ZOTE
share
face book ipyana stephen
Share
Share
instagram p yhaa tv
instagram p yhaa tv
usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

0 comments:
Post a Comment