VIDEO:MOURINHO NA EVA CARNEIRO WAKIRUSHIANA MANENO BAADA YA KUINGIA UWANJANI KWENDA KUMTIBU HAZARD
Daktari wa
timu ya Chelsea, mwanadada Eva Carneiro wiki hii amepigwa stop kuendelea kukaa
katika benchi la timu hiyo na mazoezini kwa ujumla, kutokana na kutokuelewana
na meneja wa klabu hiyo Jose Mourinho.
Katika tukio
lililotokea wikend iliyopita Chelsea wakitoa sare ya 2-2 na Swansea katika
uwanja wa Stamford Bridge, Mourinho katika hali isiyo ya kawaida, alimbwatukia
daktari huyo mwanamke kwa kile alichosema, daktari huyo alichelewesha muda wakati
timu yao inahitaji matokeo kwa kwenda kumtibu Eden Hazard ambaye Mourinho
anaamini hakuumia bali alikua kachoka.
Kauli hizi
za Mourinho zimewashangaza wengi na kuwakera wengi wa mashabiki wa klabu hiyo kwa
kumuona Mourinho amekosa busara na heshima mbele ya taaluma ya dada huyo
aliyekaa klabuni hapo tangu mwaka 2009.
Penye wengi,
pana mengi pia. Kupitia katika mitandao ya kijamii, mashabiki mbalimbali
ulimwenguni kote waliandika hisia zao kutokana na sakata hilo. Lakini kama
ilivyo kawaida, penye wengi, wapo waliomtusi kocha wao Jose Mourinho, lakini
hawakukosa waliomdhihaki mwanadada huyo kwa kuhusisha utendaji kazi wake na
jinsia yake.
Juzi, daktari
huyo aliandika kupitia ukurasa wake wa Facebook, kuwashukuru mashabiki duniani
kote kwa meseji za faraja katika wakati huu mgumu kwake.
Eva,
amefungiwa kukaa katika benchi wala kuhudhuria mazoezi ya timu yake na kocha
Jose Mourinho raia wa Ureno, ingawa ataendelea wazifa wake wa kuwa daktari
namba moja wa timu.
Wachambuzi
wa mambo ya jinsia nchini England, wanahusisha tukio hili na lile lililokuwa
kati ya kocha huyo huyo Mourinho walipozozana na mke wa kocha wa Real Madrid,
Rafael Benitez wiki iliyopita, baada ya Jose Mourinho kumkashifu Benitez kuwa ana
kitambi.
Katika ugomvi
huo na mke wa Benitez, Mourinho alimtaka mwanamke huyo kuacha kuingilia mambo
yasiyo muhusu na badala yake akamkashifu kwa kumtaka akae nyumbani na kumuandalia
chakula mumewe.
Matukio haya
yote mawili kati ya Mourinho na wanawake hawa yanaleta tafakari ya ubaguzi wa
kijiinsia 'sexism' ambao Mourinho kauanzisha katika soka.
Kwanini
lakini haya yote? Mourinho anasema alikasirishwa na kitendo cha daktari huyo
kuingia uwanjani kumtibia Eden Hazard kwa anachokiamini Mourinho kwamba Hazard
alikua kachoka. Lakini mikanda ya kipande hicho yanaonesha kwamba daktari huyo
aliitwa na mwamuzi akafanye kazi yake.
Wachambuzi
wengi wanaamini Mourinho yuko katika wakati mgumu 'stress' kutokana na
kutofanya usajili mzuri huku akitakiwa kutetea ubingwa wa ligi hiyo ya nchini England,
sanjari na kufanya vizuri katika michuano mingine, huku timu yake ikionekana
kutokuwa imara.
Makocha
wengi wamekuwa wagumu kuweka ukweli hadharani na badala yake, wamekuwa wakitafuta
mbuzi wa kumtoa kafara, ili upepo upite. Pep Guadiola pia aliwatupia lawama,
madaktari wa klabu yake ya Bayern Munich baada tu ya kula kichapo cha goli 3-1
mbele ya FC Porto ya Ureno katika michuano ya klabu bingwa ulaya mwaka jana.
Je, hali itakuwaje Stamford Bridge? Tusubiri kuona nini kitajiri siku za usoni. Je, utawala wa juu utayabariki maamuzi ya Mourinho dhidi ya daktari huyo? Na vipi timu, itapata matokeo mfululizo baada ya kuondolewa kwa daktari huyo katika benchi? Muda utasema.
Tuwe Pamoja Huku Ilikupata Stori ZOTE
share
Share
Share
instagram p yhaa tv
instagram p yhaa tv
usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos


0 comments:
Post a Comment