Ni kawaida au rahisi kwa binadamu
kuahaidi kitu katika maisha yake ila katika suala la utekelezaji ni
wachache sana wanaoweza kutimiza huenda ni kwa makusudi au bahati mbaya
wamesahau. August 28 nakusogeza karibu na mchambuzi maarufu Tanzania katika masuala ya soka Edo Kumwembe.
Edo
ni miongoni mwa watu wachache waliowahi kuweka ahadi na kuitimiza,
tarehe 23 June 2003 ni siku ambayo ipo vichwani mwa wapenda soka wengi
kwani ni siku ambayo alifariki uwanjani kiungo mahiri kutokea Cameroon Marc-Vivien Foé katika michuano ya Kombe la Mabara iliyokuwa inafanyika Lyon Ufaransa.
Tukio hilo lilitokea katika mechi kati ya Cameroon dhidi ya Colombia ni siku ambayo kila mpenda soka alishikwa na simanzi akiwemo mchambuzi mahiri wa soka Tanzania Edo Kumwembe, kwakuwa ni mtu wa soka Edo aliamua kuweka ahadi ambayo August 27 imetimiza mwaka mmoja toka ahitimize.
Edo
akiwa na mtoto wake Marc-Vivien aliyetimiza umri wa mwaka mmoja jana,
huku akiwa kamvalisha jezi ya Victor Wanyama wa Southampton
Baada ya tukio hilo Edo aliamua kusema siku atakayo bahatika kupata mtoto wa kiume basi atamuita jina la kiungo mahiri ambaye kwa sasa ni marehemu Marc-Vivien Foé.
Kinacho vutia zaidi sio tu kutimiza bali ni ahadi ambayo imetimia baada
ya miaka 12. Mwaka jana alipata mtoto wa kiume na kumuita Marc-Vivien Kumwembe.
“Sababu
kubwa iliyonifanya nimuite mwanangu jina la Marc-Vivien ni wakati
alipoanguka uwanjani na kufariki mwaka 2003 katika michuano ya mabara
ilikuwa ni mechi kati ya Cameroon dhidi ya Colombia nilikuwa nyumbani
natazama ile mechi”>>> Edo Kumwembe
“kwanza
ilikuwa mara yangu ya kwanza kuona mwanasoka mwenye jina kubwa anaanguka
uwanjani na kufariki kwa hiyo pale pale nilisema nikipata mtoto wa
kiume nitampa jina la Marc-Vivien nimefurahi nimetimiza ahadi na hata
kama angekuwa hai leo hii nakuona ahadi niliyoweka miaka 12 iliyopita
nimetimiza angesikia faraja sana” >>> Edo Kumwembe
P yhaa tv coming soon
Tuwe Pamoja Huku Ilikupata Stori ZOTE
share
face book ipyana stephen
Share
Share
instagram p yhaa tv
instagram p yhaa tv
usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

0 comments:
Post a Comment