China kuimarisha ujenzi wa mfumo wa kisasa wa mawasiliano na uchukuzi

Kongamano la pili kuhusu mikakati ya maendeleo ya sekta ya mawasliano na uchukuzi nchini China limefunguliwa  Beijing. Ofisa wa Kamati ya maendeleo na mageuzi ya China aliyehudhuria kongamano hilo Bw. Li Guoyong amesema, hatua ya mwanzo ya mtandao wa miundombinu ya mawasiliano na uchukuzi imekamilika.

Akizungumza kwenye kongamano hilo, mkaguzi wa idara ya sekta za kimsingi katika Kamati ya maendeleo na mageuzi ya China Bw. Li Guoyong amesema, katika miaka ya hivi karibuni, hatua ya mwanzo ya mtandao wa miundombinu ya mawasiliano na uchukuzi nchini China imekamilika, na vigezo vyake vingi vinachukua nafasiya kwanza duniani. 

"Inakadiriwa kuwa hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu, urefu wa jumla wa reli nchini China utafikia kilomita laki 1.2, ikiwa ni nafasi ya pili duniani baada ya Marekani. Urefu wa reli ya kasi umefikia kilomita elfu 19, ambayo inazidi urefu wa jumla wa reli ya kasi katika nchi nyingine zote duniani. Urefu wa barabara umefikia kilomita milioni 4.56, na kwa barabara ya kasi urefu wake umezidi kilomita laki 1.2, ambayo pia inachukua nafasi ya kwanza duniani.
 
 Urefu wa njia za meli katika mito mbalimbali umefikia kilomita laki 1.26, urefu wa mabomba ya kusafirishia mafuta umekuwa kilomita laki 1.2, bandari za pwani nchini China kwa ujumla zina nafasi zaidi ya 2,200 za kupokea meli zenye uzito wa tani elfu 10, na uwezo wa kushughulikia mizigo katika bandari hizo pia unachukua nafasi ya kwanza duniani.

Tuwe Pamoja Huku Ilikupata Stori ZOTE
share



Tokeo la picha la twitter

comment
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment