Wanaume wawili wanatarajiwa
kufikishwa mahakamani nchini Zimbabwe baadaye leo wakishtakiwa kwa
makosa ya uwindaji , baada ya simba maarufu nchini humo kuuawa na mtalii
mmoja raia wa Marekani .
Simba huyo,Cecil,alipigwa risasi nje kidogo ya mbuga ya wanyama
ya taifa ya Hwange na Walter Palmer, daktari wa meno na mtu anayependa
uwindaji Bwan Palmer -ambaye pia anaweza kukabiliwa na mashtaka ,
anasema anajuta kwa kumpiga risasi , lakini akasema alidhani alikua
katika mawindo halali.
Maandamano juu ya kuuawa kwa simba huyo yamefanyika nje ya makaazi ya bwana Palmer katika jimbo la Minnesota nchini Marekani .
Share
Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com
Phone:0719337774
0 comments:
Post a Comment