Birdman afanya interview aweka mezani ukweli kuhusu ugomvi wake na Lil Wayne!!
Kumekuwa na stori nyingi sana kuhusiana na ugomvi wa Lil Wayne na Birdman, tukasikia kuwa Lil Wayne anataka kuondoka Cash Money Records kwasababu Birdman hataki kumlipa hela yake.
Tukasikia ugomvi umefikishwa Mahakamani na Lil Wayne amesisitiza kuwa ataondoka na wasanii aliokuja nao, Nicki Minaj na Drake kama Birdman hatamlipa pesa anazomdai…Lil Wayne anataka dola mil. 51 (Bil 102 za Tz).
Birdman kaamua kumuita radio personality Angie Martinez nyumbani kwake Miami kufanya nae interview kuhusu ugomvi huu, Birdman alikuwa na haya ya kusema…
>>> Lil Wayne
ni mwanangu, haijalishi kumetokea nini…nataka afanye maamuzi kwa faida
na maslahi yake, nilikutana na Wayne akiwa hana chochote nikamlea kama
mwanangu na amekuwa mwanangu, mimi na yeye tuliibadilisha gemu ya rap
Marekani…<<<Birdman.
>>> Nilishawahi
kumpatia Lil Wayne mkataba wa zaidi ya dola milioni 100 na kutanguliza
dola milioni 67 za advance na mpaka leo huo ndio mkataba wa bei juu
zaidi kwenye hii industry…sasa sielewi haya maneno yanatoka wapi lakini
kama nilivyosema Wayne ni mtoto wangu atakachokifanya nitamsupport.<<< Birdman
>>> Sitaki
aondoke, lakini mpaka sasa sijasikia kauli yoyote ya yeye kutaka
kuondoka ikitoka mdomoni mwake, akinifuata na kusema baba nahisi umefika
wakati wa mimi kufanya yangu nitamruhusu, awe au asiwe na mimi yule ni
mwanangu na nitamsupport kwa kila kitu. <<<Birdman
>>> “Nilianza
hii biashara nikiwa na miaka 17 na cheque yangu ya kwanza ilitoka
Universal Records nikiwa na miaka 19 na ilikuwa ya dola
Mil.30…nimetengeneza pesa mno kwa nini nitake kumuua Lil Wayne? Nadhani
wanajaribu kutuvuta kutokana na makundi ya kibiashara alafu na nyie watu
wa media mnachochea”. <<< Birdman
>>> “Lil
Wayne akitaka kuondoka sawa nitamsupport, siwezi kumtema kisa kaachana
na mimi, kama baba haitakuwa sawa kumfanyia hivyo mwanangu… Kuhusu Nicki
Minaj na Drake,hapana wale hawataondoka na Wayne, Wayne kuondoka
haimanishi na wao wataondoka”. <<<Birdman.
>>> “Sijui
kilichotokea siku ile, mimi sikuepo mjini siku hiyo na nilisikia kuwa
basi la Lil Wayne lilipigwa rasasi, na nataka ujue kitu… mtu yoyote
akijaribu kumtishia Lil Wayne maisha basi amini mimi na huyo mtu
tutakuwa na matatizo makubwa, lakini mimi kupanga kumuua ni kitu cha
kijinga“. <<<Birdman.
Kuhusu kumwagia Lil Wayne pombe, Birdman alisema kuwa yeye hawezi kumfanyia hivyo mwanae na kwanza hawezi kufanya hivyo kwa mtu yoyote.
0 comments:
Post a Comment