Kocha
wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa Mkurugenzi wa klabu hiyo Lord
Harris ameongeza chumvi kuhusu uwezo wa kifedha wa klabu katika suala la
usajili msimu huu.
Lord
Harris alisema kuwa Arsenal ina uwezo mkubwa wa kifedha kwa sasa
kununua mchezaji wa aina yoyote isipokuwa Lionel Messi na Christiano
Ronaldo, kutokana na kuwa na kiasi cha zaidi ya pauni milioni 200 katika
akaunti.
"Lord Harris kwa kiasi fulani ameenda mbali sana kwa sababu hakuna ukweli wowote juu ya hilo",aliwaambia waandishi.
"Tupo
kaika nafasi ambapo tuko makini kuangalia kama kuna mtu sahihi
atapatikana, basi tunaweza kufanya kitu, lakini si kama ambavyo
imezungumzwa.
"Tuko katika nafasi nzuri kabisa tukiwa na kikosi bora, mimi nina furaha kwa hilo.
"Sisi
tuko makini kwa kila sehemu. Tuko makini kutafuta wachezaji tunaoweza
kuwapata. Tumetumia kiasi kikubwa sana fedha mismu miwili iliyopita na
kumleta Gabriel katikati ya msimu ambaye yuko tayari kwa mapambano sasa.

0 comments:
Post a Comment