wa na ku
Kiungo
wa Arsenal Aaron Ramsey amekiri kufurahishwa sana na taarifa za
Barcelona kumtaka huku akisema kuwa angependa siku moja akacheze
Uhispania.
Mchezaji
huyo wa kimataifa wa Wales alikuwa akihusishwa na kuhamia Camp Nou
mwanzoni kabisa mwa dirisha la usajili majira haya ya joto.
"Ni wazi kwamba ni jambo linalovutia kusikia hivyo", aliliambia Guardian".
"Barcelona
walichukua makombe matatu msimu ulioisha na ni suala la luvutia mno
kusikia unahusishwa na moja ya vilabu bora duniani."
"Siku
moja ningependa kucheza nchini Uhispania na kupata uzoefu wa pale pia.
Lakini kwa sasa nipo Arsenal na nina imani kubwa kwamba timu yangu
itafanikitoa changamoto kubwa kwa timu nyingine duniani.".

0 comments:
Post a Comment