MAMBO HAYA MAGUFULI ATAJIFUNZIA IKULU

Waziri wa Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuli.
WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuli ambaye atapeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika nafasi ya urais kwenye uchaguzi mkuu ujao, ndiye anapewa nafasi kubwa ya kurithi mikoba ya Jakaya Kikwete.

Uzoefu unaonesha kuwa mgombea anayesimama kwa tiketi ya CCM huwa katika nafasi nzuri ya kuibuka mshindi kutokana na historia, kwani wapiga kura wengi bado wana imani na chama tawala.

Hata hivyo, hali huenda ikawa tofauti sana mwaka huu, kwani vyama vya upinzani kwa umoja wao wa Ukawa, vinaonekana kuwa na nguvu inayoweza kukitikisa chama hicho, na hasa kama ‘uhamisho’ unaozungumzwa kuhusu Edward Lowassa utafanyika na mbunge huyo…
Waziri wa Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuli.
WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuli ambaye atapeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika nafasi ya urais kwenye uchaguzi mkuu ujao, ndiye anapewa nafasi kubwa ya kurithi mikoba ya Jakaya Kikwete.
Uzoefu unaonesha kuwa mgombea anayesimama kwa tiketi ya CCM huwa katika nafasi nzuri ya kuibuka mshindi kutokana na historia, kwani wapiga kura wengi bado wana imani na chama tawala.

Hata hivyo, hali huenda ikawa tofauti sana mwaka huu, kwani vyama vya upinzani kwa umoja wao wa Ukawa, vinaonekana kuwa na nguvu inayoweza kukitikisa chama hicho, na hasa kama ‘uhamisho’ unaozungumzwa kuhusu Edward Lowassa utafanyika na mbunge huyo wa Monduli kuwa mgombea wake.
Lakini wakati hayo yakisubiriwa, ni jambo zuri kumzungumzia Magufuli kutokana na uzoefu. Atashinda nafasi hiyo na atakwenda Ikulu. Licha ya urais, mbunge huyu wa Chato atasimama pia kama Mwenyekiti wa Taifa wa CCM.
Katika nafasi hiyo, bila shaka Magufuli atapata shida ya kuwaongoza watu wanaokifahamu vizuri chama hicho kuliko yeye ambaye anaonekana kama ‘wakuja’. Historia haimuoneshi kuwahi kushika nafasi yoyote ya uongozi katika chama, ukiondoa ujumbe wake wa Halmashauri Kuu (NEC).
Lakini pia Magufuli akiwa Ikulu, itampasa kujifunza uvumilivu, somo moja gumu sana ambalo kwa asili huwa ni kipaji. Ingawa tunafurahi kwa sababu tunaelekea kumpata kiongozi mtendaji, lakini tuna hofu kuu na jinsi anavyotekeleza majukumu yake, hasa ule mtindo wake wa kuwajibisha watu jukwaani.
Rais wa nchi hapaswi kuwa mtu wa kukurupuka, kwa sababu ya unyeti wa nafasi yake pamoja na madaraka yake makubwa. Kama hatakuwa mtu wa kusikiliza, kutafakari na kushauriwa, ipo hatari ya nchi kushuhudia maamuzi yatakayoandika historia.
Lakini pia Magufuli atapaswa kujifunza diplomasia. Siasa za nje ni vitu vya msingi sana katika ujenzi wa taifa lolote. Historia haimuoneshi kama mtu mwenye kufahamiana na wanasiasa wa nje, kitu ambacho kwa kiongozi wa ngazi yake ni muhimu sana.
Vyovyote iwavyo, urais wa Magufuli una vitu vingi vya msingi alivyopaswa kuwa anavijua, ambavyo bahati mbaya atakwenda kujifunzia akiwa Ikulu na hili siyo jambo dogo kama tunavyofikiria.

Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment