Habari wana familia ya mpira wenzangu. Tumeongea mengi na tumesoma mengi kuhusu kukua kwa mpira wetu Tanzania.
Binafsi naona wanachi wengi tunakosoa kuliko kutoa ushauri wa nini kifanyike.
Nimekaa
nimeona nije na ushauri huu ambao naamini pale nilipoishia kuna
Mtanzania mwenzangu atakua na jicho la ziada ataongezea au atapunguza
pale nilipozidisha au kupunguza lengo likiwa ni kujenga kuliko kulaumu
tu.
{1}.
Ili kuanza kutengeneza msingi imara wa mpira wetu,tuamue kwamba kila
timu ya ligi kuu nilazima iwe na timu C ya under 17 na tuweke ligi kuu
ya vijana hawa wa under 17 .kama huna timu hii basi unapoteza uhalali wa
kucheza ligi kuu.
{2}
kila timu ya ligi kuu ni lazima iwe na timu B yaani under 20 na tuweke
ligi kuu ya vijana wa umri huo na tutafute bingwa wake kwa msimu mzima
na kama huna timu hii unapoteza uhalali wa kushiriki ligi kuu.
{3} Mashindano haya ya vijana yasifanyike kama bonanza kuwaita sehemu moja, bali iwe ligi kama ilivyo ligi kuu.
kila
timu icheze nyumbani na ugenini na hapa kama timu yako A inayoshiriki
ligi kuu itashuka daraja basi na timu zako zote unashuka nazo kwenda
kujiunga na daraja la kwanza bila kujali timu yako B au C ilishika
nafasi ya ngapi kwenye ligi TWO au ligi TREE ili kutoa nafasi kwa zile
timu zitakazopanda zipate nafasi kwenye timu a,b na c .
{4}
Na kwa timu za daraja la kwanza pia kanuni itakua hiyo lazima uwe na
timu hizo ndio upate uhalali wa kucheza ligi daraja la kwanza.
Mimi
naamini tukisimamia vizuri na kuwa wakari na lengo moja hapa tutakua
tunatengeneza msingi imara wa soka letu na kuepuka lawama hizi
tunazotupa kwa viongozi wetu wa TFF na kocha bila kuangalia tumekwama
wapi.
Timu hizi za vijana sio ziwe kwenye makaratasi tu bali zionekane kweli zipo na jicho letu tulitupie sana huku.
Naamini
haya yakifanyika tutatumia ligi hizi kuvuna vipaji nchi nzima kwa ajili
ya timu zetu za Taifa kuanzia ile ya under 17, 19,20 na senior team.
Nchi nyingi zimeendelea duniani kwa kuacha uvivu na kuwekeza kwenye soka la namna hii na mwisho wamefanikiwa.
0 comments:
Post a Comment