ndoto za kumuoa mtoto wa Rais wa Marekani..

 
Kuna baadhi ya wanaume wana ndoto siku moja wawe na uwezo wa kumuoa mtoto wa Rais wa Marekani aitwaye Malia Obama, lakini swali je ni kweli itawezekana?
.
Mmoja mwenye ndoto kama hiyo ni wakili kutoka Kenya ambaye amesema atajitoa kwa kila hali kuhakikisha anatimiza ndoto zake za kuweza kumpata mtoto huyo huku akimuahidi Rais Barack Obama vitu mbalimbali kama mahari kwake.

http://i2.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2015/05/wakili.jpg
Kiprono Matagei amesema yupo tayari kumzawadia rais huyo ng’ombe 50, kondoo 70 na mbuzi 30 ili ampe mtoto wake Malia ambaye kwa sasa ana miaka 17.
Amesema alianza kumpenda mtoto huyo tangu mwaka 2008 wakati akiwa na miaka 10 na alikua akisubiri apate nafasi hiyo, na sasa anatumia mwanya wa Rais huyo atakapofanya ziara nchini humo mwezi ujao ili aweze kuongea naye.
 
Amesema familia yake imeridhia kumsaidia kufanikisha kumpata mtoto huyo kwa kuchangia gharama za mahari aliyoahidi kumpa Rais huyo.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook ni ipyana stephen na Instagram ni p yhaa tvkwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata.

Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment