Mwanamuziki Chantal Saroldi kutoka Italia.
Mwanamuziki
Chantal Saroldi (kushoto), akizungumza na wanahabari Dar es Salaam leo
mchana. Kulia ni Balozi wa Italia nchini, toka Italia.
Balozi wa Italia nchini, Luigi Sccoto
(kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, kuhusu
tamasha la muziki litakalofanyika kesho Hoteli ya Mediterraneo iliyopo
Kawe ambapo mwanamuziki huyo atatoa burudani.
Mkurugenzi wa Hoteli ya Mediterraneo
waandaaji wa tamasha hilo, Samantar Abdinur Lusuf (katikati),
akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni mwanamuziki Chantal Saroldi
na Mmoja wa Wakurugenzi wa Hoteli hiyo, Alas Abdinur.
Balozi wa Italia nchini, Luigi Sccoto
(wa pili kulia), akiwa meza kuu na mwanamuziki huyo. Kulia ni mpiga
kinanda wa mwanamuziki huyo Gianluca Tagliazucchi na wakurugenzi wa
hoteli hiyo waandaaji wa tamasha hilo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Dotto Mwaibale
Mwanamuziki wa miondoko ya Jazz kutoka
nchini Italia Mwenye asili ya Tanzania Chantal Saroldi anataraji
kutumbuiza katika Hafla maalumu ya kusherehekea Siku ya Taifa la Italia
ambapo raia wa Italia waishio nchini watajumuika pamoja kwenye viunga
vya ubalozi wa Italia ili kusherehekea Siku hiyo.
Mwanamuziki Chantal Saroldi mwenye
asili ya Italia na Tanzania alizaliwa nchini Tanzania katika mkoa wa
Kilimanjaro akitokea kabila la Wachaga.
Chanty yupo nchini kwa ajili ya ziara
maalumu ya Muziki ambapo kesho anatarajia kutumbuiza katika hoteli ya
Mediterraneo ya jijini Dar esalaam na Juni 2 anataraji kutumbuiza katika
hafla maalumu inayoandaliwa na ubalozi wa Italia nchini ikiwa ni
maadhimisho ya siku ya Taifa hilo.
Balozi wa Italia nchini Tanzania, Luigi
Scotto, alisema kuwa katika kuzingatia kuwa mwanadada Chantal ni
mwanamuziki mahiri waratibu wa sherehe hizo wamemchaguliwa kuja
kutumbuiza katika hafla hiyo kwa kuwa ni nembo muhimu inayoziunganisha
nchi mbili hizi za Tanzania na Italia.
Katika hatua nyingine mwanadada huyo
alisema kuwa anajilaumu kwa kutojifunza lugha ya mama yake ambayo ni
kiswahili, huku akibainisha kuwa mikakati ni kujifunza lugha ya
Kiswahili.
Mwanamuziki huyo amewahi kushinda tuzo
mbalimbali ikiwemo tuzo ya dhahabu katika kipengele cha uhariri na
uandishi wa nyimbo ikitolewa na Disc Festival.
0 comments:
Post a Comment