MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Sunday Mangu ‘Linex’, amesema tangu ameanza kujihusisha katika mapenzi hajawahi kuachana na mwanamke yeyote bila ya kuwa maadui.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Linex alisema haoni sababu ya kuwa hivyo kwasababu hakuzaliwa pamoja na mwanamke huyo lakini anashangaa imekuwa ikimtokea hivyo.
Alisema ni vizuri kumfanya mpenzi wako wa zamani awe rafiki yako wa karibu ili kuweza kubadilishana mawazo na sio kununiana kuwa kama paka na panya.
“Ukweli toka nimejua kumpenda mtoto wa kike au kuwa kwenye uhusiano sijawahi kuachana na mtu alafu mahusiano yanapokwisha yule mtu asiwe adui yangu,” alisema.
0 comments:
Post a Comment