Jokate Mwegelo:Mwanamziki Ali Kiba Ndio Kila Kitu Kwangu...ila....





MREMBO mchakarikaji Bongo,  Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, juzikati aliamua kuvunja ukimya na kusema kuwa mwanamuziki Ali Kiba kwa sasa ndiye kila kitu katika mambo yake mengi ya kimaisha.
Akizungumza na Ijumaa Jokate alisema, watu wanaongea sana kuhusiana na ukaribu wao bila kujua kuwa Kiba ni mtu wake kitambo na sasa ndiye kila kitu kwake kwani ana projekti naye kibao ambazo zinakuja na wasioelewa, ipo siku wataelewa.
 

Yaani watu wangu wajue Kiba ni kila kitu kwangu ila siyo ishu ya mapenzi, tuna projekti kibao, nawaomba watu wavute subi--ra watajionea kila kinachoendelea kati yetu.Kuanzia sasa Kiba atakuwa akipeperusha ‘brand’ za Kidoti kwa kila atakachofanya ikiwa ni pamoja na mavazi,” alisema Jokate.
TAENDELEA KUKUPATIA HABARI,PICHA NA MAELEZO,ENDELEA KUNITEMBELEA HAPA.
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment