 |
Add caption |
Samatta anayekipiga katika klabu ya TP
Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, anatajwa kuwa mmoja wa
wachezaji watanzania wanaoingiza fedha nyingi kupitia soka – akiripotiwa
kulipwa mshahara usiopungua $8000 kwa mwezi bila kuongeza marupurupu.
Mmoja ya wachezaji wa kitanzania wenye mafanikio katika soka nje ya
mipaka ya Tanzania, Mbwana Samatta leo asubuhi ameposti picha ya gari
lake jipya analotumia akiwa nchini Tanzania.
Gari
aliloposti Samatta ni Range Rover lenye rangi ya damu ya mzee ambalo
lina namba za usajili za Tanzania na linakua gari la pili la thamani
ambalo Samatta ameliweka hadharani baada ya mwaka 2013 kulionyesha gari
lake aina ya Chrysler Crossfire ambalo lilikuwa na thamani ya takribani
millioni 50 za kitanzania.
Samatta alijiunga na TP Mazembe akitokea Simba SC kwa ada ya uhamisho iliyovunja rekodi kwa kipindi hicho ya $100,000.
Kuna kitu gani Samatta amewahi kufanya uwanjani huwezi kukisahau?
Share
Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com
Phone:0719337774
0 comments:
Post a Comment