Hii ishu ya mgomo wa mabasi ya
abiria tangu mwaka 2015 umeanza imegonga vichwa vya habari kwa mara ya
pili.. mara ya kwanza ilikuwa April 2015, lakini ukaisha baada ya kama
saa 7 hivi kupita.
Jana May 5 2015
ikawa stori kubwa kwa mara ya pili, madereva wa mabasi wamegoma tena..
siku ikaisha huku kukiwa hakuna muafaka ambao umepatikana kuumaliza
mgomo huo.
Leo tena hali ikawa kama jana, daladala
na mabasi makubwa ya kwenda mikoani yote yaliendeleza mgomo.. ikafika
saa sita mchana Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda na Kiongozi wa CHADEMA, Freeman Mbowe wakaongea na viongozi wa Chama cha Madereva wakakubaliana na baadae mgomo ukaisha mabasi yakaanza safari.
Jahazi limeokolewa na Mkuu huyo wa Wilaya wa Kinondoni ambapo amewaahidi kwamba ameunda Tume ambayo itakutana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda ili kupata tamko la Serikali kuhusu madai ya madereva hao, na majibu yatapatikana kesho asubuhi kutoka Serikalini.
0 comments:
Post a Comment