ADVOCAAT HANA SHIDA NA SUNDERLAND, APANGA KUACHIA NGAZI


 
Kocha wa timu ya soka Sunderland ya England, Dick Advocaat ametangaza kubwaga manyanga kuendelea kuifundisha klabu hiyo, japokuwa kocha huyo amefanikiwa kuiokoa timu hiyo kutoka katika janga la kushuka daraja msimu huu.
 
Advocaat alijiunga klabuni hapo mwezi March mwaka huu akiziba pengo la Gus Poyet, na amesema kuwa hategemei kuendeleza ujuzi wake katika utawala wa timu hiyo. ''
 
Sunderland imekuwa ni moja ya sehemu muhimu kwenye fani yangu. Wakati fulani katika maisha yako wapaswa kufanya uamuzi" Advocaat.
 
 Kwa upande wake mwenyekiti wa Sunderland Ellis Short, amesema kuwa amefadhaishwa na taarifa ya kocha huyo lakini anaheshimu uamuzi wake huku akiahidi kuendelea kumshukuru.
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment