

Kama ni shabiki wa Liverpool najua utakuwa umesikitishwa na goli la dakika za lala salama la AFC Bournemouth lililofungwa dakika ya 90 ya mchezo na kuifanya Liverpoolkutoka uwanjani vichwa chini kwa kufungwa jumla ya goli 4-3.

Magoli ya AFC Bournemouth yalifungwa na Callum Wilson dakika ya 56 kwa penati, Ryan Fraser dakika ya 76, Steve Cook dakika ya 79 na Nathan Ake dakika ya 90, huku Liverpool walianza kupata goli mapema tu dakika ya 20 kupitia Sadio Mane, Divock Origi dakika ya 22 na Emre Can dakika ya 64.
0 comments:
Post a Comment