RAIS YAHYA JAMMEH ABADILI MAAMUZI, SASA AKATAA MATOKEO YA URAIS


Rais wa Gambia Yahya Jammeh amekataa matokeo ya uchaguzi ya urais uliofanyika mwezi huu, ikiwa ni wiki moja tu tangu akubali kushindwa.

Jammeh ameelezea sababu za kukataa matokeo hayo kuwa ni kuwapo kwa hitilafu katika upigaji kura na kutaka kuitishwa uchaguzi upya.

Jammeh, aliyeingia madarakani baada ya mapinduzi ya mwaka 1994, alishindwa na mpinzani wake Adama Barrow, ambaye alishinda kwa kura asilimia 43.
Bw. Barrow amemtuhumu rais aliyemadarakani kwa kuvunja demokrasia kutokana na kutokubali matokeo.
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment