December 13 2016 BBC wameripoti kuwa nchini Mexico utakutana na makaburi ambayo yangeweza kugeuzwa hata kuwa nyumba ambazo matajiri wengi wangejivunia kuishi. Unaambiwa ni makaburi makubwa yaliyojengwa na kuwekwa huduma za kisasa na vitu vingi vya anasa.
Kuna baadhi ya makaburi yenye viyoyozi, kuna vioo visivyopenya risasi na baadhi yana hata vyumba ambavyo wageni wanaofika kutoa heshima kwa wafu, wanaweza kuketi na kupata kila kitu kinachopatikana katika nyumba za kifahari.
Baadhi yanakadiriwa kugharimu hadi Sh milioni 633 milioni, Makaburi mengi haya hupatikana jimbo la Sinaloa, anapotokea mlanguzi mkuu Joaquin “El Chapo” Guzman ambaye kwa sasa anazuiliwa na anatarajiwa kuhamishiwa Marekani mwakani.
Katika eneo moja la makaburi, Jardines del Humaya, katika mji mkuu wa jimbo la Culiacan, ndipo unapopata baadhi ya makaburi ya kupendeza zaidi.
Kwa mujibu wa BBC kaburi moja ambalo linadaiwa kuwa na mwili wa mlanguzi aliyetumiwa kuua watu, lina hata kamera za kiusalama, pamoja na kioo kisichopenya risasi. Baadhi ya makaburi yamejengwa kama nyumba za kisasa au makanisa madogo. Krismasi inapokaribia baadhi huweka miti bandia ya Krismasi, lakini kinachokosekana katika makaburi mengi ni utambulisho wa aliyezikwa ndani.
0 comments:
Post a Comment