Kiungo wa Manchester United Henrikh Mkhitaryan atakuwa nje ya uwanja hadi Boxing Day baada ya kuumia enka hapo jana katika mchezo ambao Manchester United ilishinda goli 1-0 dhidi ya Tottenham.
Kiungo huyo raia wa Armenia ambaye ndiye aliyefunga goli hilo pekee katika mchezo huo alifanyiwa madhambi na beki wa kulia Danny Rose na kulazimika kutolewa nje ya uwanja.
Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amesema Mkhitaryan hajaumia sana, hivyo hahitaji kufanyiwa upasuaji na anatarajia kushuka dimbani siku ya Boxing Day.
Danny Rose akimfanyia madhambi Enrikh Mkhitaryan iliyopelekea kuumia enka
Kocha Jose Mourinho akipiga shuti hewa baada ya kushikwa na midadi
0 comments:
Post a Comment