Msanii wa muziki wa gospel Bahati Bukuku baada ya kuzushiwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa amefariki dunia kwa ajali, amekanusha taarifa hizo na kusema kuwa taarifa hizo zimeandaliwa na watu wanaotaka kumpunguzia mashabiki.
Bahati Bukuku amesema taarifa za kifo chake ni mbingu tu ndiyo zitajua, kwa kuwa shetani hana nafasi ya kujua taarifa za kifo chake.
“Ni watu ambao wanaamini wakiongea hivyo watanipunguzia mashabiki, mpango aliouandaa shetani hauwezi fanikiwa, kwa sababu kifo changu shetani hatatangulia kujua ila Mbingu zitajua, shetani hana sababu za kujua taarifa zangu”, Bahati Bukuku alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio.
Bahati amesema tayari ameripoti kwenye vyombo husika vya uchunguzi ili kumchukulia hatua za kisheria mtu alianzisha uzushi.
0 comments:
Post a Comment