YAYA TOURE AREJEA DIMBANI KWA KISHINDO NA KUIPATIA USHINDI MANCHESTER CITY


Yaya Toure amerejea kwa kishindo uwanjani kwa kuifungia Manchester City magoli mawili na kuipatia ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Crystal Palace.

Toure, akicheza kwa mara ya kwanza katika ligi kuu ya Uingereza kwa msimu huu baada ya kumaliza tofauti zake na kocha, alishirikiana vyema na Nolito na kufunga goli la kwanza.

Hata hivyo Crystal Palace walijibu mapigo na alikuwa Wilfried Zaha aliyemtengenezea nafasi Connor Wickham aliyetokea benchi na kusawazisha goli.

Hata hivyo Toure, ambaye hakuwa na City kwa takriban miezi mitatu alipachika goli la pili akiutumbukiza kimiani mpira wa kona uliopigwa na Kevin de Bruyne.
                        Yaya Toure akishangilia goli baada ya kutikisa wavu wa Crystal Palace 
                 Connor Wickham akifunga goli pekee la Crystal Palace katika mchezo huo 

Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment