Timu ya Leicester City imeendeleza mwenendo mzuri katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na kutinga hatua ya mtoano baada ya kuifunga Club Brugge kwa magoli 2-1.
Katika mchezo huo Leicester City ilikuwa inahitaji pointi moja tu kutinga hatua ya 16 bora lakini ikapata pointi tatu zitakazo wahakikishia kumaliza wakiwa vinara katika kundi G.
Shinji Okazaki alifunga goli safi la kwanza akiunganisha krosi ya Christian Fuchs, huku Riyad Mahrez akifunga goli la ushindi kwa shuti la penati, Jose Izquierdo alifunga goli pekee la Club Brugge.
Mpira uliopigwa na Shinji Okazaki ukitinga wavuni na kuandika goli
Riyad Mahrez akifunga goli la pili la Leicester City kwa mkwaju wa penati
0 comments:
Post a Comment