Kocha wa Arsenal Arsene Wenger na kocha wa Man United Jose Mourinho Jumamosi watakuwa wanakutana kwa mara ya kumi na sita, Jose Mourinho akiwa na vilabu viwili tofauti alikuwa na Chelsea na sasa anaifundisha Man United.
Mourinho amecheza na Arsenal ya Wenger mara 15 akiwa kafanikiwa kumfunga mara nane na kukubali kufungwa mara moja huku mara sita wakiishia kutoka sare, Wengerwamefungana na Mourinho mara 1 katika mchezo wa Ngao ya hisani, huku Wengerakifungwa mara 5 EPL, mara 2 Kombe la Ligi.
0 comments:
Post a Comment