Mrembo Hamisa Mobetto Ataja Sababu ya Wasanii wa Bongo Kukosa Tuzo za MTV Mama

Hamisa Mobetto amefunguka sababu ya wasanii wa Bongo Fleva kutofanya vizuri kwenye tuzo za MTV MAMA zilizofanyika Jumamosi ya Oktoba 22 mjini Johannesburg, Afrika Kusini.

Akiongea na mtangazaji wa kipindi cha The Playlist cha Times FM, Lil Ommy model huyo wa wimbo wa ‘Salome’ amesema kuwa team ndizo zilizochangia Tanzania ishindwe kupata hata tuzo moja.

“Unajua kwanza sisi Tanzania tuna team, kwahiyo team zinakuwa kama zinatutenganisha, kama zile team zote zingekuwa kitu kimoja labda watanzania wote tungeweza kushinda. Kuna watanzania wengine wanadiriki kuwapigia promo Instagram wanigeria washinde wao,” amesema Mobetto.

Mwanamitindo huyo ameongeza kuwa team hizi zingekuwa na faida kama zingekuwa zinaungana kwenye kitu cha kuiwakilisha nchi. Tazama mahojiano hayo hapa chini.
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment