Maneno ya ukali ya kocha wa Spurs kwa kiungo aliyesajiliwa pound milioni 30


Moja kati ya stori zinazogonga headlines za soka nchini England ni hii ya kocha wa Tottenham Hotspurs Mauricio Pochettino kuongelea uwezo wa kiungo wa kimataifa wa Ufaransa anayeichezea timu hiyo Moussa Sissoko.
Kama ambavyo hutarajiwa na wengi kuona mchezaji anayesajiliwa kwa dau kubwa mara nyingi hupata nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza kwa kiasi kikubwa, lakini kwa upande wa Moussa Sissoko aliyesajiliwa na Spurs kwa pound milioni 30 akitokea Newcastle United imekuwa tofauti kidogo.
477269595-466414
Mauricio Pochettino
Mauricio Pochettino ameweka wazi msimamo wake kuhusu kiungo huyo ambaye hadi sasa amempa nafasi ya kuanza katika mechi 5 za mashindano yote na mechi tano nyingine akitokea benchi.
“Mchezo wa mpira wa miguu sio tu unahitaji pesa, mchezaji unahitaji kuonesha uwezo katika mazoezi na kuthibitisha kuwa wewe ni bora kuliko mchezaji mwenzako ili upate nafasi ya kucheza, kama unamsajili mchezaji ina maana unatarajia kitu fulani kama hakipo kwa nini usitoe nafasi kwa mwenzake ambaye anaonesha uwezo”
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment