Mgombea wa Republican, Donald Trump ameonekana kuongoza kwa mbali katika uchaguzi wa Urais wa Marekani unaoendelea huku majimbo muhimu yakiwa yameshapiga kura.
Hillary Clinton alianza vizuri katika uchaguzi huo akiongoza lakini mambo yamebadilika na ndoto yake ya kuwa Rais wa kwanza mwanamke wa taifa kubwa zaidi duniani imeanza kufifia.
Trump ameshinda majimbo muhimu yakiwemo Ohio, Carolina Kaskazini na Florida, na sasa yamebaki majimbo 270 ya uchaguzi (electoral votes) na ana nafasi kubwa ya kuingia Ikulu.
Hadi saa tatu usubuhi hii, Trump anaongoza kwa 244 dhidi ya 215 ya Clinton, na anasubiri kupata point 26 kufikisha 270 ambazo zitampa uhakika wa kuwa Rais mpya wa Marekani.
Endelea Kufuatilia Matokeo ya Uchaguzi wa Marekani kupitia hapa hapa
0 comments:
Post a Comment