KIPENGA cha kuashiria pambano limeanza kimeshapulizwa nchi Marekani , ambapo leo sandukula kupiga kura litatoa maamuzi ya nani atakuwa mrithi wa Rais Barack Obama kati ya Hillary Clinton na Donald Trump,anaandika Faki Sosi.
Wagombea wote wawili hakuna ambaye unaweza kumtabiria zaidi ya kusubiri kura za Wamarekani kuuamua nani awe Rais wao.
Ingawa mchungaji maarufu kutoka nchini Nigeria TB Joshua amemtabiri Clinton kushinda uchaguzi huo.
Kampeni zilipamba moto , vitisho , vijembe vilitawala majukwaani katika kampeni za wagombea hao wawili lakini hadi kufikia leo hakuna jambo baya lilijitokeza nchini humo.
0 comments:
Post a Comment