DAVID SILVA AIHAKIKISHIA MANCHESTER CITY KUTIKA HATUA YA 16 BORA


Goli la kusawazisha la David Silva limeihakikishia Manchester City kutinga hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mwaka wa nne mfululizo baada ya sare ya 1-1 na Borussia Monchengladbach.

Katika mchezo huo Manchester City ilijikuta ikiwa nyuma baada ya Raffael kuachia shuti kali la umbali wa yadi 15 lililompita kipa Claudio Bravo na kutinga wavuni.

Hata hivyo goli hilo lilisawazishwa na David Silva kwa goli alilolifunga kwa kuteleza na kuutumbukiza mpira wavuni akiunganisha krosi ya chini ya Kevin de Bruyne.
                      Shuti lililopigwa na Raffael likitinga wavuni baada ya kushinda kipa Bravo 
                      Mpira uliopigwa na David Silva ukitinga wavuni na kusawazisha goli
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment