Wafungwa wapatao 25 wameuliwa katika mapambano baina ya kambi mbili hasimu kwenye gereza lenye wafungwa wengi kaskazini mwa Brazil.
Polisi nchini Brazil wamesema wafungwa saba kati ya waliokufa wamekatwa vichwa vyao na sita miongoni mwao wamechomwa moto na kufa.
Tukio hilo lililotokea huko Boa Vista, katika jimbo la Roraima, limetokea wakati wa kutembelea wafungwa katika gereza hilo.
Watu 100 waliokuwa wakitembelea wafungwa ambao walitekwa na wafungwa wakati wa mapambano hayo wamekombolewa na vikosi vya kutuliza ghasia.
0 comments:
Post a Comment