Cristiano Ronaldo amepata msaidizi katika ufungaji, wakati Ureno ikiichakaza Faroe Islands kwa magoli 6-0 katika mchezo wa kuwania kufuzu kutinga michuano ya kombe la dunia.
Kinda Andre Silva, 20, anayechezea Porto alifunga magoli matatu yaani hat-trick katika kipindi cha kwanza na kisha Ronaldo kuongeza la nne katika kipindi cha pili.
Katika dakika za mwisho Joao Moutinho aliongeza la tano huku Joao Cancelo akikamilisha goli la sita kwa Ureno.
Kinda Andre Silva akipachika goli la kwanza la Ureno
Cristiano Ronaldo akidhibitiwa na kuanguka chini
0 comments:
Post a Comment