POMBE ZA MPELEKESHA MREMBO KIDOA



 MODO anayefanya poa Bongo, Asha Salum ‘Kidoa’



MODO anayefanya poa Bongo, Asha Salum ‘Kidoa’ amefunguka kuwa wanaume aliokuwa nao kwenye uhusiano wa mapenzi kipindi cha nyuma walikuwa wakimcheka na kumdharau kwa kumuona mshamba sababu ya kutotumia pombe, jambo lililomfanya asidumu penzini.


Akipiga stori na paparazi wetu, Kidoa alisema muda mwingi alikuwa akijiona ni mwenye bahati mbaya sababu kila mwanaume aliyeingia naye kwenye uhusiano alikuwa ni mtu wa kupombeka na kumuona yeye mshamba kwa kutokunywa kama ilivyo kwa mastaa wengine, lakini sasa anamshukuru Mungu kafika panapostahili.

“Nimedharaulika sana maana watu wakikuona mtoto wa mjini halafu staa haupigi urabu basi wanakuona boya, jambo lililosababisha kutodumu nao katika mapenzi kwa kuwa tabia haziendani, lakini kwa sasa ninaye mwandani wangu ninayeishi naye nimekuwa mwenye amani sababu si mtumiaji wa hivyo vitu,” alisema Kidoa pasipo kumuanika jina mpenzi wake wa sasa.
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment