MREMBO KIDOA HANA BIFU NA AGNES MASOGANGE


kidoa
Mwanamitindo na muigizaji, Kidoa Salum amedai kumaliza bifu lake na Agnes Gerald maarufu kama Masogange.

Wawili hao waliwahi kuripotiwa kuwa na ugomvi mzito huku Kidoa akishutumiwa kutoka na mpenzi wa Masogange ambaye ni muigizaji Rammy Galis.
Akiongea na gazeti la Mtanzania, Kidoa amesema, “Ni kweli tulikuwa na bifu tena kubwa sana lakini tulikuja kukaa tukaelewana. Unajua ilivyo ni kwamba, mimi huyo bwana wake sikumtaka na wala sijawahi kutoka naye na kama ningemtaka basi mimi ningeanza kuwa naye kabla yake.”
“Ukweli ni kwamba nilikuwa karibu sana na Rammy Galis kwa sababu ya kazi na mpaka sasa tumefanya kazi nyingi ambazo zimetufanya tuwe karibu,” ameongeza.
Mwanamitindo huyo aliwahi pia kuhusishwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na rapper Cyrill Kamikaze.
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment