Polisi wamesema moto huo umetokea katika chumba cha wagonjwa mahututi kwenye hospitali ya binafsi ya SUM, mjini Bhubaneswar katika jimbo la Orissa.
Makumi ya wagonjwa wamepelekwa katika hospitali zingine katika mji huo.
Askari wa zimamoto 120 wameitwa kukabiliana na moto huo, ambao baadaye ulifanikiwa kuzimwa. Waziri Mkuu Narendra Modi ameshtushwa na tukio la moto huo.
Vikosi vya zimamoto vikipambana kuzima moto huo
0 comments:
Post a Comment