MFAMLE WA THAILAND BHUMIBOL ADULYADEJ AFARIKI DUNIA


Mfalme wa Thailand, Bhumibol Adulyadej, ambaye ni mfalme aliyekaa madaraka kwa muda mrefu, amefariki dunia baada ya kuwa mfalme kwa muda wa miaka 70.

Mfalme Adulyadej , 88, alikuwa anaheshimika mno katika nchi hiyo iliyokumbwa na migogoro ya kisiasa pamoja na mapinduzi ya mara kwa mara.

Mfalme Adulyadej amekuwa katika hali mbaya ya kiafya katika siku za hivi karibuni na ameonekana mara chache mbele ya umma.

Mfalme huyo amekufa wakati nchi ya Thailand ikiendelea kuwa chini ya uongozi wa kijeshi kufuatia mapinduzi ya mwaka 2014. 
             Wananchi wakilia kuomboleza kifo cha Mfalme wao Bhumibol Adulyadej
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment