Mtayarishaji wa muziki wa Bongo Flava, Master J, amewataja Shirko, Abby Daddy na Mesen Selekta kuwa ndio wapishi wa muziki hapa Tanzania anaowakubali zaidi.
ABYDAD
Abydad ni miongoni mwa watayarishaji muziki wanaokuja kwa kasi baada ya kufanya nyimbo kadhaa zinazofanya vizuri kwenye redio ukiwemo ‘Nagharamia’, ‘Subira’, ‘Aje’ na nyingine kibao.
MESEN SELEKTA
Producer Mesen wa De Fatality studios ambae ndiye producer pekee anayetengeneza muziki halisi wa Singeli, Baadhi ya singeli alizowahi kutengeneza nipamoja na Hainaga Ushemeji ya Man Fongo, Kazi Kazi ya Prof J na sholo Mwamba, Ghetto ya Sholo Mwamba.
SHIRKO
Nimmoja wa maprodyuza wakali ambae kashatengeza Hits kibao za Yamoto Band, Salamu TMK (Mkubwa na Wanawe).
Master J amewataja watatu hao kwa kumweka pembeni Marco Chali ili kuwa na mtazamo usiokuwa na upendeleo kwakuwa anafanya kazi kwenye studio yake, MJ Records.
Master J amedai kuwa anawakubali watayarishaji hao wa muziki kwakuwa wana uwezo wa kutengeneza kila aina ya muziki tofauti na watayarishaji wengine wengi ambao amewaita ni ‘beatmakers’.
0 comments:
Post a Comment