Mastaa wa EPL ambao hutowaona wakicheza weekend hii na waliopona majeruhi


Baada ya mapumziko ya mechi za kalenda ya FIFA na mechi za kuwania kufuzu kucheza Kombe la Dunia 2018 Urusi, weekend hii michezo ya Ligi Kuu England itaendelea kama kawaida, weekend hii kwa maana ya Jumamosi na Jumapili inatarajiwa kuchezwa michezo zaidi ya 7.
Wakati Chelsea wakiwa wanatarajia kumkosa staa wao Willian kutokana na kufiwa na mama yake, wachezaji wengine ambao wanatarajiwa kuwa nje ya uwanja ni Harry Kaneambaye bado anasumbuliwa na majeruhi, kwa upande wa Arsenal Lucas Perezatakuwepo uwanjani lakini Oliver Giroud bado majeruhi.
Kwa upande wa Man United Luke Shaw na Mkhitaryan wanaendelea vizuri licha ya kuwa waliripotiwa kutokuwa na uwezo wa kurejea uwanjani mapema, wakati hayo yakiendelea kocha wa Tottenham Hotspurs Mauricio Pochettino amethibitisha kuwa kiungo wao Moussa Dembele ni majeruhi.
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment