Timu ya Liverpool wamefungamana pointi na kinara wa Ligi Kuu ya Uingereza Manchester City baada ya kupata ushindi mzuri wa magoli 4-2 dhidi ya Crystal Palace.
Katika mchezo huo Liverpool ilipata magoli kupitia kwa Emre Can, Dejan Lovren, Joel Matip na Roberto Firmino na sasa ni tofauti ya magoli tu ndiyo inayowatenganisha wao na kinara Manchester City na timu ya pili ya Arsenal.
Licha ya kushambulia vizuri timu ya Liverpool bado ilionyesha kuwa na udhaifu katika safu ya ulinzi kufuatia kumruhusu mara mbili James McArthur kufunga magoli.
Roberto Firmino akiwa ameruka juu huku mpira alioupiga ukiingia wavuni
Wachezaji wa Liverpool wakimkubatia beki Mjerumani Joel Matip baada ya kufunga goli
0 comments:
Post a Comment