Katika mchezo wa usiku wa October 18 dhidi ya FC Copenhagen, Leicester waliibuka na ushindi wa goli 1-0 lilifungwa na mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa PFA Riyad Mahrezambaye pia ana mchango wa moja kwa moja katika kusaidia Leicester kufunga goli 4 kati ya 5 katika michuano hiyo.
Licha ya ushindi huo wa Leicester City katika uwanja wao wa King Power, imeripotiwa na BBC kuwa kufuatia kuwashwa kwa miale ya moto na shabiki wa Copenhagenkunaweza kufanya Leicester wakaadhibiwa na UEFA kutokana na kanuni.
Sheria za UEFA zinaeleza kuwa ulinzi wa uwanja kabla na wakati wa mchezo huwa ni chini ya uangalizi wa timu mwenyeji, kama Leicester itagundulika ulifanyika uzembe katika ulinzi basi inawezekana wakakumbana na adhabu kutoka UEFA.
0 comments:
Post a Comment