Staa anayepamba video za wasanii mbalimbali wa Bongo Fleva a.k.a Video Queen, Asha Salum ‘Kidoa’ amefunguka kuwa malipo kidogo anayopata kutokana na kazi hiyo yamemfanya aamue kukaa pembeni na kugeukia uigizaji.Akizungumza na Gumzo la Town la Mtanzania
Jumamosi, Kidoa amesema kwa sasa yupo bize zaidi katika uigizaji wa tamthilia na filamu mbalimbali.
Anasema: “Hakuna kitu kwenye u-Video Vixen, tunalipwa kidogo sana. Kwa sasa sitaki tena. Naweza kusema hakuna cha maana zaidi ya kuonekana… lakini kama mtu akija na pesa ya maana, naweza kushiriki kwenye video yake.”Alipoulizwa pesa ya maana ni kiwango gani, haraka alisema: “Pesa ya kueleweka. Nimechoka kufanya kazi isiyokuwa na malengo, mtu akija na milioni yake, naingia mzigoni. Chini ya milioni moja, sishiriki video ya msanii kabisa.”“Niseme ukweli, kwa sasa najivunia nimekuwa hot cake kwenye tamthilia… natafutwa sana na ninafanya kazi hata tano ilimradi tukubaliane.
“Ujue tamthilia na filamu wananilipa vizuri sana, pesa ambayo sijawahi kulipwa na ninahisi huko kwenye video za wasanii sikuwahi kufikiria kupata fedha kama hizi, ndiyo maana nimefumbuka macho na kuitambua thamani yangu,” anasema.
Anasema pamoja na kwamba kwa sasa amepata
mapokezi mazuri na makubwa kwenye tamthilia na filamu, awali walimgomea wakidhani hana kipaji.
“Mimi kipaji changu hasa ni uigizaji, sikuwa na ndoto za kuwa Video Vixen kabisa. Niliwafuata baadhi ya wasanii na watayarishaji wakubwa lakini walinitosha wakiamini labda sina kipaji, lakini leo hii wameona uwezo wangu wamenikubali.
“Siwezi kukataa kuwa video za wasanii wa
Bongo Fleva zimenisaidia, kwakweli zimenitoa lakini hazilipi. Maisha siyo kuonekana tu, lazima uwe na kitu unaingiza ndiyo utaona raha ya kazi,” anasema Kidoa ambaye video ya Akadumba
ya msanii Ney wa Mitego ndiyo iliyomtambulisha.
0 comments:
Post a Comment