KATIBU MKUU WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI PROFESA JUSTIN NTALIKWA AFANYA ZIARA KATIKA KIWANDA CHA KUCHAKATA GESI CHA MADIMBA – MTWARA

 Meneja Mradi wa Kiwanda cha Kuchakata Gesi cha Madimba,  Sultan Pwaga ( wa pili kutoka  kulia mbele) akimwongoza Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa ( wa tatu kutoka kulia mbele) kwenye ziara ya kukagua kituo hicho ili kujionea shughuli zake.
 Meneja Mradi wa Kiwanda cha Kuchakata Gesi cha Madimba,  Sultan Pwaga akielezea shughuli za kiwanda hicho mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa (hayupo pichani)
 Meneja Mradi wa Kiwanda cha Kuchakata Gesi cha Madimba,  Sultan Pwaga (kulia) akifafanua jambo kwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa (kushoto) katika ziara hiyo.
 Eneo la mwanzo  la bomba la kusafirisha  gesi kuelekea Dar es Salaam  kupitia Mtwara, Lindi na Pwani kama linavyoonekana
pichani.
 Sehemu ya kiwanda cha kuchakata gesi cha Madimba kama inayoonekana pichani.
 Meneja Mradi wa Kiwanda cha Kuchakata Gesi cha Madimba,  Sultan Pwaga (kushoto) akitoa maelezo hukusu
mikakati inayofanywa na kiwanda hicho katika kuhakikisha kuwa gesi ya uhakika inapatikana kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa (kulia)
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa akisaini kitabu cha
wageni mara baada ya kuwasili katika chumba cha kuongozea mitambo (control room) katika kiwanda cha kuchakata gesi cha Madimba.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa (kushoto)
akifuatilia maelezo
  ya namna ya uendeshaji wa  mitambo ya kuchakata gesi  ya Madimba yaliyokuwa yanatolewa na  Stanslaus Malya (hayupo pichani)
 Mtaalam kutoka kiwanda cha kuchakata gesi  cha Madimba, Stanslaus Malya akionyesha uongozwaji wa mitambo unavyofanywa katika
kiwanda cha kuchakata gesi 
 cha Madimba.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa (waliokaa mbele katikati) na Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) Kapuulya Msomba ( kushoto waliokaa mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na
wataalam wa kiwanda cha kuchakata gesi cha Madimba na wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) na TPDC.
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment