BAADA ya ukimya wa muda mrefu kutawala kuhusu ujauzito alionao mrembo anayesumbua Bongo, Hamisa Mobeto, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ameibuka na kukiri kuwa mimba ya mrembo huyo imeharibika.
Diamond aliyekuwa akitajwa kuwa mhusika wa kiumbe hicho, alifunguka hayo kupitia Kipindi cha D’ Wikend Chart kinachorushwa na Runinga ya Clouds mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo pamoja na mambo mengine aliyozungumza, alikanusha taarifa za yeye kuwa mhusika lakini akakiri kwamba mrembo huyo alikuwa mjauzito na sasa mimba imeharibika. “Mimi mwenyewe nilikuwa sijui kama ana mimba lakini ndiyo hivyo tena imeharibika so yupo kwenye wakati mgumu. Tumpe pole na tumpe pole pia aliyekuwa mhusika wa kiumbe hicho.
Mimi si mhusika bwana, hata wakati tunashuti naye Salome nilikuwa sijui kama ni mjamzito lakini ndiyo hivyo kwa sasa hatuna budi kumuombea arudi katika hali yake ya kawaida,” alisikika Diamond. Ijumaa Wikienda lilimvutia waya Mobeto ili kuweza kumsikia kama ana lolote kuhusu ishu hiyo, simu yake iliita bila majibu.
Ujauzito wa Mobeto ulikuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii ambapo wengi waliamini mhusika ni Diamond kitendo ambacho kilisababisha maneno kumfikia mpenzi wa staa huyo, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ na kutibua hali ya hewa lakini kwa sasa mambo yako shwari baada ya Zari kuelewa kwamba Mobeto hana madhara
0 comments:
Post a Comment