BRAZIL YAIBUKA NA USHINDI BILA YA KUWA NA NEYMAR


Timu ya taifa ya Brazil imeweza kuongoza katika kuwania kufuzu michuano ya kombe la dunia 2018 kwa mataifa ya Amerika ya Kusini, baada ya kushinda magoli 2-0 dhidi ya Venezuela katika mchezo uliochezwa huku mvua zikinyesha na kusimama kwa nusu saa katika dimba la Merida.

Mabingwa hao mara tano wa kombe la dunia ambao walicheza bila mshambuliaji wao Neymar walipata goli la kwanza ndani ya dakika nane ambalo lilionekana lilitokana na mzaha na kufungwa vizuri.

Kipa wa Venezuela Daniel Hernandez alijaribu kumpasia mpira beki wake lakini, Gabriel Jesus aliuwahi na kisha kuunyanyua mpira juu ya kipa huyo kwa umbali wa mita 20 na kufunga goli zuri. Willian alifunga goli la pili la Brazil.
                                    Mchezaji wa Chelsea Willian akiifungia Brazil goli la pili 
Mashabiki wakitumia tochi za simu zao kupata mwanga baada ya taa kuzimika kwenye uwanja wa Merida
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment