Kampuni ya Bakhresa Foods imedhamiria kuongeza viwanda vingine vya usindikaji hapa nchini ili kuongeza thamani kwa mazao ya wakulimu. Ahadi hiyo imetolewa na mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo, Said Salim Bakhresa.
Ametoa kauli hiyo alipokutana na waziri mkuu, Kassim Majaliwa jijini Dar es Salaam. Bakhresa amesema ana mpango wa kujenga kiwanda kimoja kwenye mikoa ya kanda ya ziwa na kwamba wamefikia uamuzi huo baada ya kuona kuwa watu wanapata usumbufu wa kuisafirisha matunda hadi Dar es salaam kwaajili ya soko.
Kwa upande wake wake waziri mkuu amemhakikishia kwamba nia ya serikali ya awamu ya tano ni kushirikiana na wafanya biashara na wamiliki wa viwanda kutokana na dhamira ya kukuza uchumi wa Tanzania kupitia uzalishaji wa viwandani na kumtaka mfanya biashara huyo kuangalia maeneo mengine ya kuwekeza kwenye sekta za hoteli na utalii ili kukuza uchumi wa nchi.
Kampuni hiyo yenye matawi Rwanda, Burundi,Msumbiji,Malawi,Zimbabwe na Afrika ya Kusini inatengeneza vyakula mbalimbali ikiwemo juice,soda, maji,biscuit,ice cream,vyakula vya nafaka vya ngano,mahindi,mchele na bidhaa za kuokwa.
BY:EMMY MWAIPOPO
0 comments:
Post a Comment