ARSENAL YAICHAKAZA SUNDERLAND NA KUZIDI KUCHAFUA KITUMBUA CHA MOYES


Timu ya Arsenal imeongeza pesha kwa kocha wa Sunderland David Moyes baada ya kupata ushindi mzuri wa magoli 4-1 dhidi ya timu hiyo na kuifanya iendelee kubakia chini ya msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza.

Katika mchezo huo Alexis Sanchez aliipatia Arsenal goli la kuongoza baada ya kumpita beki Lamine Kone na kutumbukiza kwa kichwa mpira wa krosi uliopigwa na Alex Oxlade-Chamberlain.

Arsenal walioutawala mpira walijikutwa wakinyimwa penati baada ya Sanchez kuonekana kuangushwa, na kisha baadaye Jermain Defoe kusawazisha kwa mkwaju wa penati baada ya kipa Petr Cech kumfanyia madhambi Duncan Watmore.

Hata hivyo Arsenal waliongeza magoli mengine matatu ya haraka ndani ya dakika sita na sekunde 20, yaliyofungwa na Olivier Giroud magoli mawili na Sanchezi goli moja. 
  Olivier Giroud akiwa ameruka juu na kuupiga mpira kwa kichwa uliojaa wavuni na kuandika goli
         Alexis Sanchez akiwa amempoteza maboya kipa wa Sunderland na kufunga goli
Share on Google Plus

About Unknown

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia; Email: Epyanastephene@gmail.com Phone:0719337774

0 comments:

Post a Comment